*HIVI UNAJUA IMANI NI MIWANI YA KIROHO?* šŸ˜ŽšŸ˜ŽšŸ˜ŽšŸ˜Ž

Mwl.Faraja Gasto

Bwana Yesu asifiwe!!!

Yamkin unaweza ukabaki umeshangaa kichwa cha somo, naamini kadri utakavyojifunza utanielewa.

Nataka nikutafakarishe kuhusu Miwani, Miwani ni kifaa kilichotengenezwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali kutegemeana na aina ya imani, kwa mfano kuna miwani zinazotengenezwa ili kumuwezesha mtu kuona mbali ikiwa ana shida ya macho, miwani zingine humuwezesha mtu kusoma maandishi madogo, miwani zingine ni maalumu kwa ajili ya kuzuia vumbi au cheche za vyuma n.k

KATIKA ULIMWENGU WA ROHO IKO HIVI
Mtu mwenye imani huwa anaonekana kama mtu ambaye amevaa miwani ambayo inamuwezesha kuona vitu mbalimbali ikiwemo kuona uwepo wa vitu katika ulimwengu wa mwili ambavyo kiuhalisia havipo ila kwa kuwa mtu anaona kupitia imani anakuwa na uhakika kuwa alichokiona kwa imani kitatokea katika mazingira ya ulimwengu wa damu na nyama.

(waebrania 11:1)
"IMANI ni kuwa na hakika ya mambo YATARAJIWAYO ni BAYANA ya mambo yasiyoonekana"

Maana yake ni kwamba mtu mwenye imani huwa ni kama mtu ambaye amevaa miwani katika namna ya kiroho kwa hiyo anakuwa na uwezo wa kuona mambo ambayo katika namna ya kawaida asingeweza kuona.

Amini tu utaanza kuona kwa namna ya tofauti.

Chapisha Maoni

0 Maoni