Hii ni maalumu kwa wachungaji na maaskofu.
Kanisa ni ofisi ya Mungu, lakini kuna wakati shetani anaweza kutumia ofisi za Mungu kutenda kazi zake kwa njia mbalimbali, njia mojawapo ni kukuletea watu wa aina mbalimbali ikiwemo matajiri.
SHETANI anaweza kukuletea matajiri kanisani ili kutekeleza kazi za shetani kanisani kwa lengo la kuharibu kanisa la Mungu.
Matajiri hao wanaweza kujitoa kwa kazi mbalimbali kama kumtunza mchungaji, kujenga jengo la ibada, kununua vifaa vya sauti na muziki nakadhalika LAKINI KUNA MAMBO SHETANI ANAKUWA AMEYAKUSUDIA IKIWEMO KUUTEKA AU KUUKAMATA MOYO WA MCHUNGAJI.
Matajiri hao wakishateka au kukamata moyo wa Mchungaji, wataanza kuingiza mambo ya kishetani kwenye moyo wa mchungaji kupitia mawazo fulani (watakupa mawazo fulani) yatakayokuharibu wewe mchungaji na kuharibu kanisa.
Kumbuka kuwa kuna watu shetani anawapa utajiri kwa ajili ya kuharibu kazi za Mungu ikiwemo kuharibu kanisa na kuangamiza watumishi wa Mungu, rejea (Mathayo 4:8-10).
Kumbuka kuwa hata Mungu huwapa watu utajiri kwa ajili ya kuimarisha maagano fulani ikiwemo kueneza ufalme wake, rejea (Kumbukumbu la torati 8:18).
(Mathayo 6:21)
Yesu alisema hazina ya mtu ilipo ndipo na moyo wake utakuwepo, kwa hiyo kama mtu amepewa utajiri na shetani akauleta utajiri huo utumike kanisani kujenga majengo, kumtunza mchungaji, kununua vifaa vya kanisa nakadhalika, MOYO WA SHETANI UTAKUWEPO KANISANI HAPO KWA KUWA HAZINA YAKE IKO HAPO KUPITIA UTAJIRI WA MTU FULANI.
Moyo wa shetani ukiwa kanisani, tarajia kuwa kazi za shetani zitafanyika hapo kanisani, mapenzi ya shetani yatafanyika hapo kanisani yaani NI USHETANI KATIKA OFISI YA MUNGU.
Angalizo: Sijasema hatupaswi kuwa na matajiri kanisani, ila nimekutazamisha jinsi shetani anavyotenda kazi zake kupitia matajiri ambao amewapa yeye utajiri.
UWE MACHO MCHUNGAJI AU ASKOFU "si kila utajiri unatoka kwa Mungu"

0 Maoni