FUATA MALISHO


 Zaburi 100:3 

Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu; ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake; tu watu wake, na kondoo wa malisho yake. 

Usiende kanisani kwa sababu kuna waimbaji wazuri, kuna muziki mzuri, kuna mabinti warembo, kuna vijana wa kiume ambao anaweza tokea mmoja wa kukuoa, kuna jengo zuri, kuna matajiri wanaoweza kukuajiri, kuna viongozi wa serikali au wakuu wa idara za serikali, kuna ratiba fupi za ibada nakadhalika.

NENDA KANISANI KUFUATA MALISHO 

Malisho ni nini?

Ni neno la Mungu au mafundisho sahihi ya neno la Mungu yanayokubadilisha na kukufanya kuwa mtu bora kwenye kila eneo la maisha yako, yanayokujenga, yanayokuimarisha, yanayoamsha na kupanda vitu vya kiungu ndani yako, yanayokuongezea kiu ya kumujua Mungu, kumtumikia, kutembea katika njia zake, mafundisho yanayokufanya umjue sana Mungu sio kujua sana hiyo dini, kumjua sana huyo mwangalizi wa kanisa hilo au dhehebu hilo nakadhalika.

NASISITIZA

1. Ni heri uwe kwenye kanisa ambalo wanakutania chini ya mti, hawana vyombo vya muziki, hawana kwaya, hawana program za kuvutia LAKINI KUNA MALISHO.

2. Ni heri uchungwe na mchungaji ambaye hana elimu rasmi za kidunia LAKINI ANA CHAKULA CHA KUKULISHA.

3. Ni heri uende kwenye kanisa ambalo liko mbali sana lakini KUNA MALISHO.

HITIMISHO

Ni jambo jema kuwa na majengo mazuri ya kukutania (majengo ya kanisa), ni jambo jema kuwa na vifaa vizuri kanisani nakadhalika.

Lakini lililo jema zaidi ni MALISHO.

👉KAMA HAKUNA MALISHO HAMA HILO KANISA HARAKA SANA KWA USALAMA WAKO NAAM KAMA HAKUNA MALISHO HAMA KATAFUTE MALISHO 🏃🏃🏃


Chapisha Maoni

0 Maoni