USHETANI KATIA OFISI YA MUNGU - Seh ya 1


 Mtu wa ujuzi wa mema na mabaya haukuwa mti wa shetani, ulikuwa mti wa Mungu kwa kuwa ndiye aliyeuweka pale (Mwanzo 2:9).

Adamu na mkewe walikula tunda la mti ule kwa maelekezo ya shetani, jambo hilo liliingiza ushetani kwenye mioyo yao na duniani.

NATAKA NIKUFUNDISHE HILI

Shetani akishindwa kukuzuia usimtumikie Mungu au akishindwa kukutoa kwenye ofisi ya Mungu (utumishi) atahakikisha unamtumikia Mungu kwa maelekezo yake au kwa nguvu zake (shetani).

Ni sawa na kuwa kwenye ofisi ya umma ila unatenda mambo kwa maslahi yako binafsi au maslahi ya watu fulani ila sio maslahi ya umma.

Ndicho shetani anachofanya, atahakikisha unakuwa kwenye ofisi ya Mungu (utumishi) ila unatenda anachokuelekeza yeye au unatenda kazi kwa nguvu zake shetani (unafanya ushetani ukiwa kwenye ofisi ya Mungu).

(Mathayo 7:21-23).


Chapisha Maoni

0 Maoni