KAZI NA WAJIBU WA MCHUNGAJI


 UTANGULIZI

Kwanza nataka ufahamu kuwa kuna tofauti ya kazi na wajibu, kazi sio wajibu na wajibu sio kazi ila ndani ya kazi kuna wajibu unaopaswa kutekelezwa.

Kwa mfano kazi ya mahakama sio kuhukumu watu, kazi ya mahakama ni kutenda haki au kumpatia mshitaki na mshitakiwa haki yake, katika kufanya kazi hiyo ndipo mahakama hutoa hukumu mbalimbali.

Mfano mwingine ni kwamba kazi ya jeshi la nchi sio kupigana vita ila kazi ya majeshi mengi ni kulinda mipaka na kulinda katiba ya nchi, kazi ya jeshi la polisi sio kukamata watu na kuwapeleka mahakamani, kazi ya jeshi la polisi ni kulinda raia na mali zao, kudumisha usalama ila katika kufanya kazi hiyo wana wajibu wa kukamata wahalifu na kuwapeleka mahakamani.

Watu wengi hudhani kazi ya mchungaji ni kuongoza na kusimamia ibada, kubatiza, kuwapa watu ushirika mtakatifu (meza ya Bwana) nakadhalika, hiyo sio kazi ya mchungaji.

KAZI YA MCHUNGAJI NI NINI?

Kazi ya mchungaji ni kulisha kondoo, rejea vitabu hivi (Yeremia 23:2,4)(Ezekieli 34:2,10)(Zekaria 11:4-7)(Yohana 21:14-17)(Zaburi 23:1-2)(Yeremia 3:15)(Zaburi 78:70-71)(Ezekieli 34:23)(Isaya 40:11).

Wachungaji hulisha watu maarifa, ufahamu au neno la Mungu (Yeremia 3:15)(Yohana 17:14).

WAJIBU WA MCHUNGAJI WA KONDOO (WATU WA MUNGU) NI UPI?

Wachungaji wana wajibu wa aina mbili, kuna wajibu wa kidini au kimadhehebu na kuna wajibu wa mchungaji kwa mujibu wa Biblia, nitaeleza kwa ufupi au kidogo kuhusu wajibu wa mchungaji kama ifuatavyo;-

1. Kulinda kondoo dhidi ya watu wabaya, mafundisho potofu nakadhalika (Yohana 17:12)(Ezekieli 34:7)(1 Samweli 17:34-36)(Yeremia 31:10).

2. Kuwatafuta na kuwarudisha kundini kondoo waliopotea (Ezekieli 34:8,12) (Luka 15:4) kutokuwatafuta kondoo wa Mungu ni dhambi.

3. Kuwahurumia kondoo au kuonyesha huruma kwa kondoo (Zekaria 11:5) kutokuhurumia kondoo ni dhambi.

4. Kuwaongoza kondoo kwenye njia sahihi (Zaburi 23:1-2)(Yohana 10:2-4).

5. Kuwaombea kondoo mambo mbalimbali kwa Mungu (Yohana 17:9-11).

6. Kuwajua kondoo kwa majina yao (Yohana 10:3,14).

7. Kuwafuatilia kondoo (Luka 15:4) kufuatilia ni kuhakikisha unajua wako wapi, kwa nini hawapo kundini, ni mambo gani yanayowakabili nakadhalika.

8. Kukusanya kondoo, asipokuwepo mchungaji kondoo hutawanyika (Mathayo 9:36)(Ezekieli 34:12)(2 Mambo ya nyakati 18:16).



Chapisha Maoni

0 Maoni