KWELI 6 KUHUSU UCHUNGAJI NA MCHUNGAJI


 1. Uchungaji ni kazi (Zaburi 78:70-72).

2. Uchungaji hauanzii kanisani au madhabahuni, uchungaji unaanzia moyoni. 

Biblia inasema Mungu alimchagua Daudi awe mchungaji wa taifa la Israeli (Zaburi 78:70-72) Mungu alimchagua Daudi kutokana na moyo wake sio uwezo wake (1 Samweli 16:7,11-12).

(Yohana 21:15-17) kabla Yesu hajazungumza kuhusu uchungaji alimuuliza Mtume Petro "wanipenda? Petro alipojibu nakupenda ndipo Yesu alizungumza kuhusu uchungaji.

Suala la kupenda ni la moyo, pia suala la kuchunga linaanzia moyoni, linaanza na kumpenda Mungu na kuwapenda kondoo.

3. Mungu ndiye huwapa watu wachungaji (Yeremia 23:4)(Yeremia 3:15)(Waefeso 4:11)(Zaburi 78:70-71).

4. Kazi kuu ya mchungaji ni kulisha kondoo (Yeremia 23:2,4)(Ezekieli 34:2,10)(Zekaria 11:4-7)(Yohana 21:14-17)(Zaburi 23:1-2)(Yeremia 3:15)(Zaburi 78:70-71)(Ezekieli 34:23)(Isaya 40:11).

5. Mchungaji huchunga kondoo, wanaochungwa ni kondoo, sio mbwa mwitu au kitu kingine. Mungu akikupa kazi ya kuchunga anakuwa amekupa kazi ya kuchunga kondoo sio mbwa mwitu au kitu kingine.

Wajibu wa mchungaji sio kuchunga dhambi, ni kuchunga kondoo.

6. Si kila mchungaji ni mchungaji wa kanisa la mahali pamoja, kuna wengine ni wachungaji wa kanisa la mahali pamoja, kuna wengine ni wachungaji wa taifa, kuna wengine ni wachungaji wa vijana, kuna wengine ni wachungaji wa wanawake, kuna wengine ni wachungaji wa akina baba, wengine ni wachungaji wa watoto, NADHANI UTAKUWA UMESHTUKA.

Rejea mifano hii ili unielewe zaidi.

(Zaburi 78:70-72) Daudi alichaguliwa na Mungu kuwa mchungaji wa taifa lote la Israeli. 

(Yohana 21:15-17) Mtume Petro alikuwa mchungaji wa kondoo za Yesu kule kwenye taifa la Israeli ila sio kwa mataifa.

(Isaya 44:28) Mungu alisema Mfalme Koreshi ni mchungaji.

TATIZO LIKO HAPA

Watu wengi hufanya huduma na kazi za Mungu kwa mapokeo na mazoea ya kidini au kimadhehebu ILA HAWAMSIKILIZI MUNGU AMEWAITIA NINI.



Chapisha Maoni

0 Maoni