KIFUNIKO KIMOJAWAPO CHA UADUI


 Adui si mtu anayekutakia mabaya au anayekutendea mabaya tu, adui ni mtu yeyote anayekutendea mema ila akiwa na nia mbaya.

Kwa mfano sisi wanadamu tukitaka kutega panya, wakati mwingine tunawawekea panya chakula lakini ndani ya chakula tunaweka sumu, panya akija hudhani kuwa anapendwa au watu wanamjali hatimaye anakula chakula bila kufahamu kuwa ule wema ni kifuniko cha uadui.

Kwa mfano mpinga Kristo atakapoanza kazi zake rasmi atakuja kama mtu wa amani, mpenda haki, mtatuaji wa matatizo, mpatanishi lakini ghafla atajifunua rasmi, atajidhihirisha kama adui wa wanadamu.

Fumbua macho yako, si kila wema ni wa amani na usalama, wema mwingine ni kifuniko cha uadui uliofichika.

Chapisha Maoni

0 Maoni