YESU WA MICHONGO - YESU WA FURSA


  

Yesu Kristo aliwaambia wakina Petro jinsi ya kufanya ili wapate samaki (pesa) rejea kitabu cha Luka 5:3-

Yesu alimwambia Petro jambo la kufanya ili apate pesa ya kulipa kodi (Mathayo 17:24-27

Unakumbuka ile habari ya Nabii Elisha na mjane, mjane alipewa ufunuo fulani uliowaokoa watoto wake wasiwe watumwa na ufunuo ule ukamtoa yule mwanamke kwenye kilio kilichotokana na deni 2 Wafalme 4:1-

👉Watu wa Mungu tusiwe tunaambiana kila wakati mambo ya mbinguni tu, mara oooooh tutaota mabawa tutaruka kama ndege wa angani tukamlaki Yesu, mara oooooh mbinguni hatutaona njaa, tutasifu na kuabudu milele, mara ooooh tutafutwa machozi, mara oooooh mbinguni hakiingii kinyonge, mara ooooh tutapewa miili mipya...........................

👉Bado tuko duniani hatujaenda mbinguni, tupeane michongo ya kupata pesa, mshtue mwenzako kuna fursa gani umeziona mahali fulani

👉Yesu tunamtaka na pesa tunazitaka, jambo la kuzingatia ni kwamba mwambie mwenzio au wenzio njia halali za kupata pesa, waambie fursa ambazo ni halali

MCHONGO PESA

Chapisha Maoni

0 Maoni