Si kila anayetoa wazo zuri ana nia njema, kuna watu hutoa mawazo mazuri lakini sio kwa nia njema.
(Yohana 12:3-6) Yuda Iskariote alipoona Yesu anapakwa marashi yenye thamani kubwa, alisema ni heri hayo marashi yangeuzwa kisha pesa hizo wakapewa masikini, ALITOA WAZO ZURI KABISA LAKINI NIA YAKE HAIKUWA NJEMA.
(1 Samweli 18:20-29)
Mfalme Sauli alitoa wazo kwamba Daudi amuoe Mikali binti wa Mfalme Sauli, wazo la Mfalme Sauli lilikuwa zuri Daudi apate mke (kupata mke sio jambo baya) LAKINI NIA YA MFALME SAULI HAIKUWA NJEMA.
👉Uwe makini na mawazo ya watu.

0 Maoni