Ukiyatazama hayo maneno mawili (kusema na kunena) unaweza kudhani yanafanana au yana maana moja lakini maneno hayo yanamaanisha mambo mawili tofauti.
KUNENA ni kuzungumzia jambo au kitu fulani au kuongelea kitu au jambo fulani.
KUSEMA ni jinsi utakavyozungumzia kitu au jambo fulani au ni jinsi unavyozungumzia kitu au jambo fulani.
(Yohana 12:49)
Kwa sababu mimi sikunena kwa nafsi yangu tu; bali Baba aliyenipeleka, yeye mwenyewe ameniagiza NITAKAYONENA na NITAKAYOSEMA.
(John 12:49)
For I have not spoken on My own authority; but the Father who sent Me gave Me a command, WHAT I SHOULD SAY and WHAT I SHOULD SPEAK (NKJV).

0 Maoni