KUKAMATA MIOYO YA WANANCHI: MBINU MOJAWAPO YA KIUTAWALA


✍Faraja Gasto

(1 Wafalme 12:25-30)

Mfalme Yeroboamu alifahamu siri za ujuzi kuhusu utawala, alifahamu kuwa ukitaka kuwatawala wananchi lazima uiteke mioyo yao.

Bahati mbaya ni kwamba mbinu aliyoitumia kukamata mioyo ya watu ilikuwa mbaya sana.

BAADHI YA MBINU ZA KUKAMATA MIOYO YA WANANCHI

(1 Wafalme 12:6-7)

● Kuwatumikia watu - kuwahangahikia.

● Kuwasikiliza na kuwajibu maswali yao.

● Kuwapa maneno mazuri - hotuba nzuri zenye maneno ya kuwatia moyo na kuwapa matumaini.

HITIMISHO

Kuna ujuzi wa utawala (administrative skills) unaofundishwa kwenye Biblia ambao hautaupata wala hautafundishwa kwenye chuo chochote kwenye hii sayari ya dunia isipokuwa utaupata utakaposoma Biblia.

Kiongozi yeyote asiyejua namna ya kukamata mioyo ya watu huishia kuwa dikteta na mkatili kabisa kwa wananchi.

Ukitaka wananchi waendelee kukukubali usitumie nguvu, kamata mioyo yao.

Ukitaka wananchi waendelee kukuamini na kukupenda usitumie nguvu, kamata mioyo yao.

Mungu na shetani  wakitaka kuwatawala watu huwa wanahakikisha wanaipata mioyo yao na kuikamata.

NB: Soma Biblia kwa utawala bora.

Chapisha Maoni

0 Maoni