UKIFAHAMU HILI LITAKUSAIDIA SANA


 Nimehudhuria vipindi vya maombi sehemu mbalimbali (makanisani, kwenye makongamano nakadhalika) KUNA BAA NIMELIONA CHINI YA JUA NALO NI HILI 👇👇👇

Wakati mwingine watu wakiwa kwenye vipindi vya maombi sio ajabu kusikia watu au mtu akisema "MUNGU MIMI SISTAHILI MBELE ZAKO AU SIFAI MBELE ZAKO"

Neno hilo linadhihirisha kuwa MTU AU WATU HAWAFAHAMU KAZI ALIYOFANYA YESU KULE GOLGOTHA ALIPOTUNDIKWA MSALABANI. 

Au yamkini wanafahamu Yesu alichofanya ILA HAWAAMINI KATIKA KAZI YA YESU ALIYOFANYA PALE MSALABANI.

UNAPASWA KUFAHAMU KUWA 

1. Ukimwamini Yesu unahesabiwa haki bure kabisa, WEWE NI MWENYE HAKI (Warumi 3:23-25).

2. Haukufanya jitihada yoyote ili upate wokovu.

(Waefeso 2:8-9) Kwa maana MMEOKOLEWA KWA NEEMA, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala SI KWA MATENDO, mtu awaye yote asije akajisifu. 

NAHITIMISHA

Usirudie tena kumwambia Mungu haustahili mbele zake. 

Kama umemwamini Yesu, WEWE UNASTAHILI MBELE ZA MUNGU.

TUMESTAHILISHWA.

Chapisha Maoni

0 Maoni