ALIYE UPANDE WETU NA ALIYE KINYUME CHETU


 (Marko 9:38-40)

Lengo la somo hili ni kuwabaini watu ambao wako kinyume nasi na kuimarisha umoja wetu.

Kama ilivyoandikwa kwenye kitabu cha Marko 9:38-40, Mitume wa Yesu waliona mtu anatumia jina la Yesu kutoa pepo wakamkataza kwa sababu alikuwa hafuatani nao, Yesu aliposikia habari hiyo aliwaambia "msimkataze kutumia jina langu kutoa pepo kwa kuwa ASIYE KINYUME CHETU YU UPANDE WETU"

Maana yake ni nini kusema ASIYE KINYUME CHETU YU UPANDE WETU?

1. Asiye kinyume chetu anafanya tunachofanya.

2. Asiyefanya tunachofanya yuko kinyume chetu.

3. Aliye upande wetu na aliye kinyume chetu tutamtambua kwa kile anachofanya, kama anafanya tunachofanya basi yuko upande wetu kama hafanyi tunachofanya basi yuko kinyume chetu.

4. Mtu anaweza kuwa mbali nasi kimwili au hafuatani nasi au hayupo pamoja nasi lakini akawa upande wetu, mtu anaweza kuwa karibu yetu kimwili, anafuatana nasi yuko pamoja nasi lakini akawa kinyume nasi.

---Mitume waliona mtu anatumia jina la Yesu kutoa pepo wakamkataza kwa kuwa hafuatani nao lakini Yesu alisema huyo mtu yuko upande wetu japo hafuatani nasi.

5. Bwana Yesu ndiye anawafahamu vizuri walio upande wetu na walio kinyume nasi kwa kuwa yeye ndiye ajuaye mioyo ya watu.

---Mara nyingi au mara zote huwa tunadhani walio karibu nasi au wanaoambatana nasi wako upande wetu, wale wasiofuatana nasi au wasioambatana nasi wako kinyume chetu hata Mitume wa Yesu walidhani kwa kuwa yule anayetumia jina la Yesu hafuatani nao basi hayuko upande wao LAKINI YESU ALIWAAMBIA MSIMKATAZE KUTUMIA JINA LANGU KWA KUWA YUKO UPANDE WETU JAPO HAFUATANI NASI.

HITIMISHO

Kuambatana nasi au kuwa pamoja nasi haimaanishi uko upande wetu, walio upande wetu wanafanya tunachofanya hata kama wako mbali nasi kimwili (hawaonekani kufuatana nasi au kuambatana nasi).

Tutawabaini walio kinyume nasi kwa kile wanachofanya, kama wanafanya kinyume na tunachofanya basi wako kinyume nasi hata kama wapo nasi kimwili (wako karibu nasi, wanaaambatana nasi, wanaitwa wakristo wenzetu).

Walio upande wa Yesu wanafanya anachofanya Yesu, wasiofanya anachofanya Yesu wako kinyume na Yesu hata kama wanaitwa wakristo au watumishi wa Kristo.

Kanisa lolote au dhehebu lolote linalotenda kinyume na kile Yesu anachofanya basi kanisa hilo au dhehebu hilo liko kinyume na ukristo hata kama lina jina la Kikristo au linajitambulisha kama dhehebu au kanisa la Kristo.

Yesu mwenyewe alisema anachofanya ni kile alichomwona Baba yake anafanya (Yohana 5:19-23), Yesu hakufanya chochote ambacho kiko kinyume na Baba yake.

Chapisha Maoni

0 Maoni