MAOMBI YA VITA ❌


 Kwenye Biblia hakuna mada au fundisho kuhusu maombi ya vita japokuwa imezoeleka kusikia mtu akisema nafundisha kuhusu maombi ya vita au tunakwenda kufanya maombi ya vita.

Najua umeshtuka sana 😜😜😜

Ndio, nilichosema kiko sahihi kabisa, sasa acha hasira fuatana nami nikusahihishe.

1. Kwenye Biblia kuna mafundisho mengi sana kuhusu VITA VYA KIMWILI NA VITA VYA KIROHO.

2. Ukitaja neno "MAOMBI" unapata picha kwamba "kuna MUOMBAJI na ANAYEOMBWA"

3. Ukisema kuna maombi ya vita unakuwa umetumia lugha isiyo sahihi kabisa, HAKUNA MAOMBI YA VITA KWA MUJIBU WA BIBLIA ILA KUNA VITA AU VITA VYA KIROHO.

NIHITIMISHE

Badala ya kuwaambia watu kwamba tunataka tufanye maombi ya vita au tujifunze kuhusu maombi ya vita, WAAMBIE WATU NATAKA TUFANYE VITA VYA KIROHO AU TUJIFUNZE KUHUSU VITA VYA KIROHO.

TUJISAHIHISHE.

Chapisha Maoni

0 Maoni