UKIFAHAMU HILI HAUTATUMIA MUDA VIBAYA


Kuna maombi ya aina nyingi sana ambayo Mungu hawezi kuyajibu.

Aina mojawapo ya maombi ni KUMUOMBA MUNGU ARUDISHE MUDA NYUMA.

Ukifahamu kuwa Mungu hawezi kujibu ombi la namna hii basi zingatia yafuatayo;

1. Tumia muda vizuri.

2. Hakikisha unayatafakari maamuzi unayotaka kuyafanya kuhusu mambo mbalimbali kabla haujafanya maamuzi hayo.

3. Maisha yamefungwa kwenye muda, namna unavyotumia muda ni tafsiri ya aina ya maisha utakayokuwa nayo wakati ujao (kama unatumia muda vibaya basi majuto yatakuwa fungu lako kwa wakati ujao, kama wewe ni mtu ufanyaye maamuzi bila kutafakari basi majuto yatakuwa fungu lako siku zijazo).

FANYA HIVI

Kama imeshatokea ulitumia muda vibaya au ulifanya maamuzi ambayo yanakugharimu, unajiona mkosaji, umejaa hatia moyoni, umejaa majuto, msongo wa mawazo nakadhalika.

1. Kubali imeshatokea na hakuna unachoweza kukibadilisha.

2. Nyamazisha sauti ya hatia moyoni mwako kwa kujisamehe na kuwasamehe watu waliosababisha umejipata kwenye majuto. 

3. Muombe Mungu akusamehe na akusaidie kusonga mbele.

Chapisha Maoni

0 Maoni