Injili ya mapinduzi ni injili ambayo inalenga kumega kanisa fulani au kuvunja kanisa fulani ili kuanzisha kanisa lingine au injili ambayo inawatoa watu kwenye injili halisi ili wawe wakristo vuguvugu au baridi kabisa nakadhalika.
Injili za namna hiyo zimekuwa nyingi sana, si ajabu mtu kuvunja kanisa fulani au kumega kanisa fulani ili akaanzishe kanisa lingine.
Mimi nimetumia neno "injili ya mapinduzi" ili kukurahisishia kuelewa, yamkini na wewe unaweza kuwa na jina lingine la kuziita injili za namna hiyo.
Injili za namna hiyo zimepigwa marufuku kwenye Biblia, Mtume Paulo alienda mbali zaidi akasema atakayehubiri injili isiyo ya Mungu NA ALAANIWE (Wagalatia 1:8).
Mara nyingi watu wanaohubiri injili za namna hiyo, kitu kimojawapo wanachotaka ni "mapato ya aibu" au kujipatia mapato haramu au mapato kwa njia isiyo halali.
Tito 1:11. Hao wanapindua watu wa nyumba nzima, wakifundisha yasiyowapasa kwa ajili ya mapato ya aibu.
TUJIHADHARI NA INJILI ZA NAMNA HIYO kwa kuwa zinaleta laana, zinaharibu watu na zinasababisha watu kukufuru.

0 Maoni