Aliyepigana vita ni Yoshua na watu aliokuwa anawaongoza vitani lakini kilichosababisha Yoshua na watu wake wapate ushindi au washindwe ni mikono ya Musa, alipoinua mikono yake waisraeli walishinda, aliposhusha mikono yake waisraeli walishindwa (Kutoka 17:10-13).
Musa alipochoka kuinua mikono yake, walikuwepo watu wa kumsaidia ili ainue mikono yake, ushindi wa waisraeli ulikuwa mikononi mwa Musa sio katika uwezo wao wa kupigana.
MAMBO KADHAA YA KUJIFUNZA
1. Wakati mwingine mafanikio yetu huwa hayatokani na juhudi zetu wenyewe bali mikono ya watu wengine, HESHIMU WATU.
2. Unapotambua mikono ya mtu fulani inasababisha unafanikiwa, ITEGEMEZE MIKONO HIYO KWA NAMNA MBALIMBALI, Haruni na Huri walipogundua ushindi wa waisraeli unatokana na mikono ya Musa walihakikisha Musa hashushi mikono chini (Kutoka 17:12-13).
Potifa alipogundua kuwa anafanikiwa kutokana na mikono ya Yusufu, alimkabidhi Yusufu miradi yake yote aisimamie (Mwanzo 39:3-6).

0 Maoni