FAHAMU HAYA MACHACHE KUHUSU KUTENDA MEMA


 Kama kutenda mema sio mojawapo ya vipaumbele vyako basi nataka nikufahamishe mambo baadhi kuhusu kutenda mema;-

1. Kutenda mema ni kupanda mbegu ambayo itakuzalia matunda mbalimbali (Wagalatia 6:9).

2. Kutenda mema ni sadaka mojawapo inayompendeza Mungu (Waebrania 23:16).

3. Kutenda mema ni mbinu mojawapo ya kuziba vinywa vya watu wapumbavu (1 Petro 2:15).

4. Kutenda mema ni silaha mojawapo ya kukabiliana na maadui zako (Warumi 12:19-21).

5. Kutenda mema ni kushiriki tabia ya Mungu (Luka 6:35).

BAADHI YA FAIDA ZA KUTENDA MEMA

1. Utavuna ulichopanda.

2. Sababu mojawapo iliyopelekea Dorcasi akafufuliwa ni Matendo yake mema (kuwashonea wajane nguo) Matendo ya Mitume 9:36:41.

✍️Kama kutenda mema sio kipaumbele chako, basi ANZA SASA.

Chapisha Maoni

0 Maoni