Kila mtu ana maadui zake yamkini wapo anaowajua pia wapo asiowajua, kutokana na mambo ambayo walitenda au wametenda maadui hao, watu wengi hujikuta wakiwatamkia mambo mabaya au wakiwaombea mambo mabaya watu hao ambao wamekuwa maadui.
Mungu huwa anashughulika na maadui zetu kwa njia mbalimbali ikiwemo kujifunua kwao au kujifunua kwa maadui zetu.
BAADHI YA MIFANO KUHUSU MUNGU ALIVYOJIFUNUA KWA MAADUI WA WATU MBALIMBALI
1. Sauli
Sauli alilitesa kanisa kwa viwango vikubwa sana nadhani wapo waliokuwa wakimwomba Mungu amuangamize Sauli lakini Mungu hakumuua Sauli ila Mungu alijifunua kwake wakati anaelekea Dameski (Matendo 9:1-17).
Mungu alipojifunua kwa Sauli ndio ulikuwa mwisho wa Sauli kulitesa kanisa la Mungu hatimaye Sauli akawa mhubiri wa injili.
2. Mfalme Nebukadneza
Mfalme Nebukadneza aliamuru wakina Mishaeli, Hanania na Azaria ambao walipewa majina mapya Shadraka, Meshaki na Abednego wauawe kwenye tanuru la moto lakini Mungu hakumuua Mfalme Nebukadneza ila alijifunua pale Babeli mbele ya Mfalme Nebukadneza (Danieli 3:1-30).
Mungu alipojifunua kwa maadui wa Hanania, Mishaeli na Azaria hatimaye heshima ya hao watu iliongezeka sana, Mungu wao aliheshimiwa kwa kuwa Mfalme alitoa amri kwamba "mtu yeyote atakayenena neno baya kuhusu Mungu wa Hanania, Mishaeli na Azaria atauawa na nyumba yake itateketezwa kabisa.
HITIMISHO
Jizoeze kumuomba Mungu ajifunue kwa maadui zako, Mungu akijifunua kwa maadui zako maadui wanaweza kugeuka kuwa marafiki, maadui wanaokuchukia wanaweza kukupenda, maadui wanaokupinga wanaweza kugeuka na kukuunga mkono.
Omba Mungu ajifunue kwa adui zako.
0 Maoni