1. Baadhi ya mambo ambayo Mungu hufundisha
2. Namna unavyoweza kufundishwa na Mungu
3. Baadhi ya faida za kufundishwa na Mungu
UTANGULIZI
BIblia inaeleza bayana kuwa Mungu amekuwa akifundisha watu tangu zamani sana hata Sasa Mungu anaendelea kufundisha mambo mbalimbali, rejea vitabu vifuatavyo (Isaya 48:17) (Yeremia 32:33)(Hosea 11:3)(Mathayo 4:23)(Marko 1:22).
BAADHI YA MAMBO AMBAYO MUNGU HUFUNDISHA
1. Mungu hufundisha namna ya kunena na mambo ya kunena.
(Luka 12:11-12) (Kutoka 4:12) Mungu hufundisha watu jinsi ya kunena na mambo wanayopaswa kunena katika mazingira tofauti tofauti.
Kuna wakati mtu anaweza kujikuta katika mazingira ambayo hajui aseme nini au ajibu nini, Mungu anaweza kukufundisha cha kunena.
2. Mungu hufundisha vita.
Jina mojawapo la Mungu tunalloliona kwenye Biblia ni BWANA WA MAJESHI (Isaya 51:16), Mungu ni mwalimu wa vita za aina zote (vita za kiroho au za kimwili).
Mungu alimfundisha vita Daudi (Zaburi 18:34)
Mungu alimfundisha vita Musa namna ya kukabiliana na wachawi na waganga wa nchini Misri (Kutoka 7:8-12)
Gideoni alifundishwa na Mungu namna ya kukabiliana na wamidiani waliowatesa (Waamuzi sura ya sita na ya saba)
Mungu anaweza kukufundisha namna ya kukabiliana na maadui wote (shetani, wanadamu, magonjwa nakadhalika)
3. Mungu hufundisha namna ya kupata faida.
(Isaya 48:17)
Kila mtu hutaka faida katika yale anayoyafanya (Mathayo 25:27)
Serikali hutaka kupata faida (Danieli 6:1-2)
Mungu ndiye mwalimu bora anaweza kukufundisha namna ya kupata faida katika biashara nakadhalika.
4. Mungu hufundisha njia sahihi ambayo mtu hupaswa kuiendea.
(Zaburi 32:8)
Biblia inaeleza bayana Mithali 14:12 "Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti".
Mungu ndiye anayeweza kukufundisha njia unayopaswa kuiendea.
5. Mungu hufundisha mambo ya maisha, ibada, ufalme wake, maombi, utu nakadhalika, rejea kitabu cha Mathayo sura ya tano, sita na Saba.
NAMNA UNAVYOWEZA KUFUNDISHWA NA MUNGU
1. Soma Biblia au jifunze neno la Mungu kwa kusoma au kusikiliza.
Unaposoma neno la Mungu, Mungu hukufundisha (Matendo ya Mitume 17:10-12)
Unaposikiliza neno lake, Mungu hukufundisha (Nehemia 8:1-9).
2. Muombe Mungu akufundishe.
(Luka 11:1-4)
Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kusali baada ya kupokea ombi la mwanafunzi wake mmojawapo.
Kama kuna jambo unataka Mungu akufundishe, basi muombe Mungu akufundishe.
3. Waendee watumishi wa Mungu au wasikilize watumishi wa Mungu.
(Kumbukumbu la torati 17:8-11)(Matendo ya Mitume 13:7)
BAADHI YA FAIDA ZA KUFUNDISHWA NA MUNGU
1. Utapata faida (Isaya 48:17)
2. Utakuwa mshindi katika vita zote (Zaburi 18:34)
3. Utakuwa na maarifa na hekima (Mithali 2:6)
4. Utapata raha nafsini mwako (Mathayo 11:29)
0 Maoni