BAADHI YA MAMBO YA KUZINGATIA IKIWA UNAHITAJI KUISHI MAISHA YA KUMTEGEMEA MUNGU


1. Epuka kuzitegemea akili zako.

(Mithali 3:5-6) Biblia haijazuia kutumia akili ila Biblia inasema "usizitegemee akili zako bali umtumaini Bwana Mungu kwa moyo wako wote" 

Haupaswi kuzitegemea akili zako kwa kuwa akili zako zitakuletea hofu, kutokuamini, kujiona dhaifu nakadhalika.

Kwa mfano kama wana wa Israeli wangezitegemea akili zao wasingeweza kupita pale kwenye mji wa Yeriko, kwa kuwa wasingeweza kukabiliana na watu wa Yeriko kutokana na mazingira ya mji yalivyokuwa, kwa kuwa walimtegemea Mungu, Mungu aliwapa mbinu ya kuwafanya wapite pale Yeriko (Yoshua 6:1-24)

Kama wana wa Israeli wangezitegemea akili zao wasingeweza kupita pale kwenye bahari ya Shamu wasingeweza kupita pale, jeshi la Misri lingewakuta pale na wangerudishwa tena utumwani lakini Musa kwa kuwa alimtumaini Mungu, Mungu alimwambia namna wanavyoweza kupata njia kwenye bahari ya Shamu (Kutoka 14:1-31)

Ukizitegemea akili zako utagundua adui zako wana nguvu kuliko wewe na hauwezi kukabiliana nao ukiwatathmini Kwa ajili zako huwezi kupata ujasiri wa kupigana nao ndio maana wale wapelelezi kumi waliwavunja moyo waisraeli kwamba hawawezi kuimiliki nchi ya Kanaani kwa kuwa wenyeji wa kule ni watu hodari (Hesabu 13:27-33)

Ukizitegemea akili zako utagundua kuwa Daudi asingeweza kupigana na Goliathi kwa kuwa Goliathi alikuwa mtu wa vita sana kuliko Daudi lakini Daudi hakuzitegemea akili zake katika kukabiliana na Goliathi.

2. Ondoa macho yako kwa wanadamu mtazame Mungu peke yake.

(Esta 4:14) "Kwa maana wewe ukinyamaza kabisa wakati huu, ndipo kutakapowatokea Wayahudi msaada na wokovu kwa njia nyingine; ila wewe utaangamia pamoja na mlango wote wa baba yako; walakini ni nani ajuaye kama wewe hukuujia ufalme kwa ajili ya wakati kama huo"

Hayo ni maneno ya Mordekai aliyomwambia Malkia Esta, Mordekai hakuweka macho yake kwa Esta Kwa sababu ni Malkia atawasaidia wasiuawe, Mordekai alikuwa anamtegemea Mungu, alikuwa anaamini kwamba hata Malkia Esta asipotililia maanani suala la wayahudi kuuawa basi Mungu anaweza kuwaokoa wayahudi kwa njia nyingine.

Ni vema ujifunze kuwa hata kama una mtu wa kukusaidia, kukukingia kifua, wa kukusemea nakadhalika haupaswi kuweka macho yako kwa wanadamu.

(Zaburi 121:1-9) Daudi alisema alingalia hukohuko lakini hakupata msaada ila alipomtazama Mungu alipata msaada.

3. Uwe mtendaji wa neno la Mungu na muombaji.

Mtu anayemtegemea Mungu hawezi kujitenga na neno la Mungu, ikiwa unataka kuishi maisha ya kumtegemea Mungu hakikisha unakuwa mtendaji wa neno la Mungu.

(Luka 5:4-6) Mtume Petro alimwambia Yesu "kwa neno lako nitashusha nyavu" na alipotendea kazi neno la Mungu aliona jambo la ajabu likitendeka kwenye kazi yake ya mikono.


 

Chapisha Maoni

0 Maoni