●Kiongozi, fahamu kuwa hauwezi kupendwa na kila mtu pia hauwezi kuchukiwa na kila mtu, hauwezi kuungwa mkono na kila mtu na hauwezi kukataliwa na kila mtu, ikitokea ukaanza kung'ang'ana kupendwa na kukubalika kwa kila mtu au ukaanza kupambana na wasiokupenda au wasiokuunga mkono HIYO NI ISHARA KUWA HUWEZI KUWA KIONGOZI BORA.
●Kukosolewa ni jambo mojawapo linalomtokea kila kiongozi kwa kuwa WANADAMU TUNAKOSEA NDIO MAANA TUNAKOSOLEWA. KUKOSOLEWA NI KUSAHIHISHWA TU (KILA MSAHIHISHAJI KUNA NAMNA ANAVYOSAHIHISHA - kuna mwingine atakusahihisha huku anakusimanga, mwingine atakusahihisha kwa kukuelekeza, kuna mwingine atakusahihisha huku anakupiga) PAMOJA NA YOTE HAYO HAKIKISHA UNAKUBALI KUKOSOLEWA, ukikataa kukosolewa NI SAWA NA KUWATANGAZIA WATU KUWA WEWE NI MUNGU (TUNAJUA NI MUNGU TU ASIYEKOSEA), kama wewe sio Mungu KUBALI KUKOSOLEWA.
●Unapokuwa kiongozi hakikisha unajua kudhibiti hasira, usipojua namna ya kudhibiti hasira tarajia kuingia kwenye orodha ya viongozi wabaya.
●Kati ya akili unazotakiwa kuwa nazo unapokuwa kiongozi NI AKILI ZA KUJUA NYAKATI, akili za kujua nyakati zinakusaidia kujua cha kufanya. Hata ukiwa kiongozi mzuri kiasi gani huwa inafika wakati watu unawaongoza wanakukinai hawataki kuongozwa na wewe wanataka mtu mwingine awaongoze USIWACHUKIE WATU HAO (WAKATI NDIO UNASABABISHA HAYO) ukifika wakati huo kama una akili za kujua nyakati utajua HUU NI WAKATI WANGU WA KUACHIA NGAZI ILI KUPISHA MTU MWINGINE ASHIKE HATAMU. Kutokana na kutokua na akili za kujua nyakati ndio maana viongozi wengine huishia kuwa madikteta, unalazimisha kuongoza watu wasiokupenda au wasiokukubali.
Naishia hapa, nitaendelea wakati mwingine.
0 Maoni