NAMNA YA KUKABILIANA NA TATIZO LA KUKOSA USINGIZI


 UTANGULIZI

Tafiti mbalimbali za kisayansi zinaonyesha kuwa usingizi una faida mbalimbali za kisaikolojia na kimwili, ndio maana tunahimizwa kulala usingizi.

Biblia inaonyesha kuwa kuna faida mbalimbali za usingizi pia zipo hasara za usingizi kutegemeana na chanzo cha usingizi (usingizi una vyanzo vyake).

Japokuwa usingizi una faida mbalimbali lakini

watu wengi hujikuta wamepata tatizo la kukosa usingizi, wengine hufanya mambo mbalimbali ikiwemo kumeza dawa mbalimbali ili wapate usingizi lakini hawapati usingizi.

Kila mtu anapaswa kufahamu kuwa zipo sababu mbalimbali zinazosababisha watu kukosa usingizi, sababu kuu ni SABABU ZA KIROHO (Mungu na shetani).

Kwa mfano Mungu alipotaka kumuinua Mordekai alihakikisha Mfalme Ahasuero anakosa usingizi ili asome kitabu cha kumbukumbu ambamo ataona taarifa za jambo jema alilofanya Mordekai (Esta 6:1-12).

Mfano wa pili ni kwamba shetani huwaondolea watu usingizi kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuwatesa na kuwafanya watende mambo mabaya (Mithali 4:16).

Hivyo basi kuna vyanzo vikuu viwili vinavyosababisha watu kukosa usingizi (Mungu na shetani).

MAMBO YA KUFANYA IKIWA UNA TATIZO LA KUKOSA USINGIZI

1. Muombe Mungu akupe kujua au akusaidie kujua kinachosababisha ukose usingizi.

- Nimetangulia kueleza kuwa Mfalme Ahasuero hakupata usingizi kwa kuwa Mungu alimuondolea usingizi ili asome kitabu cha kumbukumbu (Esta 6:1-12).

Ikiwa Mungu ndiye anakuondolea usingizi basi kuna jambo anataka ufanye, muombe akupe kujua unachopaswa kufanya.

2. Kemea roho ya kuzimu inayosababisha ukose usingizi.

- Nimetangulia kukueleza kuwa shetani naye huwaondolea watu usingizi kwa sababu mbalimbali (Mithali 4:16).

Hivyo basi unaweza kukemea au kufunga kazi za roho chafu inayosababisha ukose usingizi.


HITIMISHO

Kama umekuwa na tatizo la kukosa usingizi unaweza kufanya hayo niliyoeleza hapo juu yatakusaidia.


Chapisha Maoni

0 Maoni