MUNGU ALIPOMWAMBIA MUSA NIMESHUKA


 MUNGU ALIPOMWAMBIA MUSA NIMESHUKA (Kutoka 3:7-8) maana yake ni kwamba jambo ambalo limemfanya ashuke;-

1. Hata kama wakiandamana, jambo hilo haliwezi kupata ufumbuzi ndio maana ameamua kushuka mwenyewe.

2. Jambo hilo haliwezi kupata ufumbuzi kwa uwezo wa kibinadamu ndio maana anaamua kushuka mwenyewe ili ampe mwanadamu uwezo wa ziada kushughulikia jambo hilo (Kutoka 4:17)

3. Ni yeye anayeweza kukabiliana na ugumu wa mioyo unaosababisha mambo mbalimbali kutokea au kuwepo kwenye nchi ikiwemo suala la mateso ya waisraeli.

4. Linahitaji mtu wa kumtumia ili lipate ufumbuzi, ni kweli Mungu alishuka lakini wana wa Israeli hawakutoka Misri ILA MUSA ALIPOKUBALI KUTUMIWA NA MUNGU hatimaye wana wa Israeli walitoka Misri, Mungu akishuka halafu akakosa mtu wa kumtumia au akakosa mtu wa kufanya naye kazi HAKUNA KITAKACHOBADILIKA, HAKUNA TATIZO LITAKALOPATA UFUMBUZI.

NB:

a). Tumuite Mungu ashuke kwenye nchi zetu.

b). Tuwe tayari kutumiwa na Mungu kwa ajili ya maslahi ya nchi zetu au mataifa yetu, NI KWELI MUNGU ANAWEZA KUSHUKA ILA AKIKOSA MTU WA KUMTUMIA KUSHUGHULIKIA MAMBO MBALIMBALI AU AKIKOSA MTU WA KUFANYA NAYE KAZI, HAKUNA KITAKACHOBADILIKA AU HAKUNA TATIZO LITAKALOPATA UFUMBUZI.

Ezekieli 22:30.

 "NAMI NIKATAFUTA MTU miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu"

---------------

Chapisha Maoni

0 Maoni