Mungu hafanyi kazi na kila mtu bali anafanya kazi na watu wenye moyo safi.
Kigezo kimojawapo ambacho Mungu hukiangalia ili afanye kazi na mtu ni MOYO SAFI.
Ifahamike kuwa kuna tofauti kubwa kati ya MUNGU KUMTUMIA MTU na MUNGU KUFANYA KAZI NA MTU, MUNGU ANAWEZA KUKUTUMIA TU ILA HAIMAANISHI ANAFANYA KAZI NA WEWE.
Sasa usishangae Yesu anaposema kuna siku atawaambia watu wengine hawajui japo watu hao walifanya miujiza mingi, walitoa unabii na kutoa pepo kwa jina la Yesu (Mathayo 7:22-23).
Kilichosababisha Mungu atake kufanya kazi na Daudi ni MOYO WA DAUDI (1 Samweli 16:1,6).
Daudi alijua siri hii kuhusu moyo umuhimu wa kuwa na moyo safi ndio maana aliomba hivi
"Ee Mungu uniumbie moyo safi" (Zaburi 51:10)
đŸ‘‰Endelea kufunga na kuomba, endelea kutoa sadaka nakadhalika ILA USISAHAU KUWA NA MOYO SAFI.
0 Maoni