MAOMBI YANAVYOTENGENEZA MAZINGIRA YA UPATIKANAJI WA MAJIBU

 


Kuna maombi ambayo huwa yanatengeneza MAZINGIRA YA KUPATIKANA KWA MAJIBU YA MAOMBI.

 

Kuna maombi huwa yanatengeneza njia au huwa yanatengeneza mlango wa kupitishia majibu.

 

(1 Wafalme 18:41-45)

Eliya alisikia sauti ya mvua kwa jinsi ya rohoni lakini kwa jinsi ya mwilini mvua ilikuwa haijanyesha.

Eliya alianza kuomba ili ile sauti ya mvua aliyosikia kwa jinsi ya rohoni inyeshe mvua kwa jinsi ya mwili.

 

Eliya aliomba mara saba, kuomba mara sita kulitengeneza mazingira ya mvua kunyesha, alipoomba mara ya saba akapata taarifa kuwa kuna dalili ya mvua, Eliya alipoambiwa kuna dalili ndipo akaacha kuomba kwa kuwa aliamini mvua inakwenda kunyesha, muda si mrefu mvua ilianza kunyesha.

 

(Luka 18:1-8)

Huyu mjane aliendelea kudai haki yake, kule kuendelea kudai kulitengeneza mazingira ya kupatikana kwa haki yake.

 

NB: Kama unaomba na hauoni matokeo fahamu kuwa yamkini maombi hayo YANATENGENEZA MAZINGIRA ya kupatikana kwa majibu ya maombi yako kwa hiyo USIKATE TAMAA, ENDELEA KUMUOMBA MUNGU (Luka 18:7-8)

 

Chapisha Maoni

0 Maoni