TOFAUTI YA SURA NA USO


 Ukiyatazama hayo maneno kwa haraka unaweza kudhani yanafanana, ukweli ni kwamba sura sio uso na uso sio sura.

SURA ni namna unavyoonekana au namna mtu au kitu kinavyoonekana kwa ujumla (mbele, nyuma, juu, chini, kulia na kushoto).

USO ni muonekano wa mbele au muonekano wa juu wa mtu au kitu.

KWA MFANO

1. Mungu alisema "na tumfanye mtu kwa mfano wetu, KWA SURA YETU" Mwanzo 1:26.

Alichomaanisha aliposema "KWA SURA YETU" ni kwamba alikuwa anaumba mtu ambaye VILE ANAVYOONEKANA ATAKUWA KAMA MUNGU (LIKENESS) ni kama ule msemo usemao "mtoto kama baba au alivyo mtoto ni kama baba yake" au "LIKE FATHER LIKE SON".

Haina maana wanafanana na Mungu, ila ANAVYOONEKANA NI KAMA MUNGU.

Waliosoma jiografia (geography) wanaelewa vizuri neno SURA YA NCHI (EARTH SURFACE).

Sura ya nchi maana yake ni MUONEKANO WA NCHI KWA UJUMLA AU JINSI ENEO LINAVYOONEKANA KWA UJUMLA.

2. Tunapewa taarifa "Giza lilikuwa JUU YA USO wa maji halafu Roho wa Mungu ALITULIA JUU YA USO WA MAJI" Mwanzo 1:2.

Kama nilivyokuambia USO NI MUONEKANO WA MBELE AU WA JUU wa mtu au kitu.

Maji hayana mbele wala nyuma ila yana juu na chini ndio maana maandiko yanasema ROHO AKATULIA JUU YA USO WA MAJI.

3. Mungu alimuuliza Kaini "KWA NINI USO WAKO umekunjamana? Mwanzo 4:6.

Namna Kaini alivyokuwa anaonekana kwa mbele alionekana ana ghadhabu (facial expression).

Naamini umeelewa tofauti ya uso na sura.

Chapisha Maoni

0 Maoni