Huwezi kufanikiwa hapa duniani kwa jambo lolote ikiwa hauko tayari kuumia na kulipa gharama.
👉Mwanamke ili azae lazima apate uchungu kwanza, katikati ya uchungu na maumivu mtoto huzaliwa, hata wanaojifungua kwa upasuaji nao hupitia adha ili mtoto azaliwe.
👉Unamkumbuka Nelson Mandela yule wa Afrika kusini, kabla hajafanikiwa kuwa Rais wa nchi alipitia nyakati zenye maumivu makali, hatimaye akaja kuwa Rais wa Nchi.
👉Unamkumbuka Mwl. Julius Nyerere wa Tanzania, kabla hajawa Rais wa Tanzania alipitia nyakati zenye maumivu mpaka kufika alipofika kisiasa.
IKO HIVI: Njia ya kuelekea kwenye mafaniko imesongwa na miiba, dhoruba na nyakati za maumivu hivyo basi lazima uwe tayari kuumia na kulipa gharama.
👆Hiyo ni kanuni ya kupata mafanikio katika jambo lolote hapa duniani.
0 Maoni