Sikumoja nilipanda gari ya abiria nikaketi karibu na dereva.
Wakati safari inaendelea nikasikia msukumo wa kumuomba Mungu, wakati nataka kuanza kuomba kimyakimya nikasikia sauti nyingine inaniambia hivi.
"jaribu kufikiri kama huyo dereva ana pepo halafu wewe unataka kuomba je! pepo wakiripuka itakuaje?
Nilipofikiri kitakachotokea endapo dereva atakuwa na pepo, nikapata picha ya ajali kwa kuwa pepo wakiripuka lazima dereva ataachia usukuani kwa hiyo tutapata ajali.
Baada ya kusikia sauti hiyo sikuendelea na mpango wa kuomba 🤣🤣🤣🤣🤣 maombi yaliishia pale, ukweli ni kwamba nilifanya kosa kwa kuwa sikumtii Mungu nililigundua hilo baadaye.
IKO HIVI: Wakati mwingine shetani anapigana na sisi kwa kutumia taswira (images) anazozileta kwenye nafsi zetu au anazotuonyesha kwenye nafsi zetu.
Unawakumbuka wale wapelelezi waliotumwa na Musa walisema "TULIJIONA NAFSI ZETU KAMA MAPANZI" (Hesabu 13:33) taswira walizoziona nafsini mwao ziliwavunja moyo wakakata tamaa ya kuelekea kwenye nchi ya ahadi.
Hivyo basi usikubali kile ambacho shetani anakuonyesha, kumbuka yeye ni baba wa uongo (Yohana 8:44).
Mpinge shetani (2 Wakorintho 10:3-5).
0 Maoni