NEEMA YA KUSAIDIA WAKATI WA MAHITAJI


 Vile ambavyo wengine wanavitaabikia au wamevitaabikia kwa miaka mingi, kwa muda mrefu na kwa gharama kubwa ukiwa na NEEMA YA MUNGU YA KUKUSAIDIA WAKATI WA MAHITAJI unaweza kuvipata kwa wepesi na kwa muda mfupi bila kutaabika na kutumia nguvu kubwa.

Ukiijua neema ya Mungu na umuhimu wake kwenye maisha ya wanadamu, kuna vitu utavipata kwa wepesi sana bila kuvitaabikia na kutumia nguvu.

Njia mojawapo itakayokusaidia kupata neema ya Mungu ya kukusaidia wakati wa mahitaji NI KUKIKARIBIA KITI CHA NEEMA CHA MUNGU.

Waebrania 4:16. 

"Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji"

--------------- 

Chapisha Maoni

0 Maoni