FURAHA INAYOKUANGAMIZA


 Si kila kinachokufanya ufurahi ni chema kwako, vingine vinakufanya ufurahi huku vinakuangamiza.

Si kila anayepambana kuhakikisha unakuwa na furaha ni mtu mwema kwako, wengine watasababisha ufurahi  huku wanachangia kukuangamiza.

Mfalme Ahabu alitaka kumiliki shamba la mtu fulani, akamuomba mtu yule amuuzie shamba lile au wabadilishane ampe shamba lingine lakini mtu yule akakataa.

Jambo lile lilimuhuzunisha Mfalme Ahabu akarudi kwake akiwa na huzuni, mkewe alipoona mumewe ana huzuni akataka kujua kwa nini mumewe ana huzuni, Mfalme Ahabu akamwambia mkewe jambo lililosababisha akawa na huzuni.

Ili kumfanya mumewe aondokane na huzuni, Yezebeli aliamua kumuua yule mmiliki wa kile kiwanja ili mumewe akipate kwa wepesi.

Hatimaye yule mtu aliuawa, Mfalme Ahabu akapata kile kiwanja akafurahi bila kujua kuwa jambo lile lingemeletea matatizo makubwa sana, Soma habari hiyo (1 Wafalme 21:1-25)

ANGALIZO: Usitafute furaha yako kwa kuondoa furaha ya wengine.

Si kila jambo linalokupa furaha ni jema kwako, mengine yanaangamiza.

Chapisha Maoni

0 Maoni