AINA 5 ZA MATENDO MEMA YENYE FAIDA


UTANGULIZI

Biblia imeweka wazi kuwa matendo mema yana faida au yanaweza kumpa faida mtu anayeyatenda (Tito 3:8).

Kuna aina nyingi sana za matendo mema yenye faida sana ikiwa mtu atayatenda, nitafundisha aina 5 tu za matendo mema yenye faida ikiwa mtu atayatenda.

AINA 5 ZA MATENDO MEMA 

1. KUWAKARIMU WATUMISHI WA MUNGU

(2 Wafalme 4:8-17) Ukarimu wa mwanamke mshunami na mumewe kwa mtumishi wa Mungu ulisababisha wakapata mtoto.

(Wafilipi 4:15-19) kanisa la Filipi lilimuhudumia Mtume Paulo kwa kumpeleka vitu mbalimbali.

Unaweza kuwakirimu watumishi wa Mungu kwa kufanya vile unavyoona moyoni mwako au Roho wa Mungu atakavyokuongoza.

2. KUWATENDEA MEMA WAJANE NA YATIMA.

(Yakobo 1:27) dini iliyo safi ni kuwasaidia yatima na wajane.

3. KUWASAIDIA MASIKINI.

(Zaburi 41:1-3) Zilizoandikwa hapo ni faida za kuwasaidia masikini.

Mithali 19:17.   Amhurumiaye maskini humkopesha Bwana; Naye atamlipa kwa tendo lake jema. 

4. KUJITOLEA KUFANYA MAMBO MEMA

(1 Timotheo 5:10e), yapo mambo mema ambayo mtu au watu wanaweza kujitolea kuyafanya kama vile kufanya usafi mtaani, kutatua kero fulani kwenye jamii.

(Luka 7:2-10) Biblia inasema huyu mtu alijitolea kujenga sinagogi, sababu hiyo ilipelekea mtoto wake kuponywa.

5. KULEA WATOTO WASIO NA WAZAZI AU WATOTO WANAOISHI KWENYE MAZINGIRA MAGUMU

(Esta 2:5-7) Biblia inasema Mordekai alimchukua mtoto wa mjomba wake yaani binamu yake aitwaye Esta na akamlea kama mtoto wake, wakati Mordekai anamchukua Esta hakujua kwamba ipo siku atakuwa Malkia.

Unaweza kulea watoto wasio na wazazi au wanaoishi kwenye mazingira magumu kwenye mji wako au kwa kuwapatia mahitaji yao kule waliko (kwenye vituo maalumu vya kuwalea).

Huwezi kujua mtoto unayemlea atakuwa nani siku za usoni.

HITIMISHO

Unaweza kufanya matendo mema mengine yaliyoandikwa kwenye Biblia na yale ambayo Roho wa Mungu atakuongoza kuyatenda.

 

Chapisha Maoni

0 Maoni