Si kila mwanamke huwa anajua kwamba kuna kazi za Mungu na za shetani hufanyika ndani ya matumbo yao, pata nafasi ya kusoma (Wagalatia 1:15)(Yeremia 1:4-5)(Mwanzo 25:23)(Waamuzi 13:5)(Zaburi 22:10)(Zaburi 58:3)(Isaya 46:3)(Isaya 49:1)(Luka 1:15)(Matendo ya mitume 14:3).
MAMBO BAADHI AMBAYO UNAPASWA KUFAHAMU KUHUSU TUMBO LA UZAZI LA MWANAMKE
1. Mtoto huumbwa kwenye tumbo la mwanamke (Yeremia 1:5)(Zaburi 139:13).
2. Tumbo la mwanamke (mama yako) lina uhusiano na wewe kwa kuwa kuna vitu vya kiroho na kimwili ulipokea kupitia tumbo lake au kuna vitu vya kimwili na kiroho vilikupata ukiwa tumboni mwake na ukazaliwa navyo. Wote tunafahamu kuwa mtoto anapokuwa tumboni huwa anaunganishwa na mama yake, huwa anapata chakula kupitia mama yake, vivyo hivyo mtoto anaweza kupokea vitu vya kiroho kupitia tumbo la mama yake au wakati akiwa kwenye tumbo la mama yake (Luka 1:15)(Isaya 49:1)(Matendo ya mitume 14:3)
3. Tumbo la mwanamke linaweza kufungwa au kufunguliwa, likifungwa hawezi kuzaa, likifunguliwa anaweza kuzaa. (Mwanzo 20:18 )(Mwanzo 16:2)(1 Samweli 1:5)
4. Tumbo la mwanamke ni mji, mtoto anaweza kuishi huko bila shida na akapata huduma zote anazotaka, kwenye sayansi utasikia neno hili "mji wa mimba".
5. Tumbo la mwanamke linaweza kuwa kaburi, kila mimba ikitungwa itatoka tu au mtoto atazaliwa akiwa amekufa (Yeremia 20:17)
6. Tumbo la mwanamke linaweza kulaaniwa au kubarikiwa
HIVYO BASI
1. Mkeo akiwa na mimba jizoeze kuombea tumbo lake ili shetani asifanye kazi zake kwenye tumbo hilo na kwa mtoto aliyemo ndani ya tumbo.
2. Kama wewe ni binti ambaye haujazaa jizoeze kuliombea tumbo lako ili shetani asifanye kazi zake huko.
3. Unapobeba mimba jizoeze kuombea tumbo lako na hicho kiumbe kilichomo ndani yako ili shetani asifanye kazi zake humo ndani.
4. Kuna haja ya kuombea matumbo ya wanawake ili shetani asiyatumie kupitisha vitu vyake, kuna haja ya kuombea wajawazito ili shetani asifanye kazi kwa watoto waliomo ndani ya matumbo ya wanawake.
0 Maoni