Kuna tofauti ya haya maneno mawili "HOMA KUPONA" na "HOMA KUMWACHA MTU"
Kama homa ilimwacha ni dhahiri kuwa homa ilimshika, kama homa ilimshika ni dhahiri kuwa kuna mahali ilitoka.
Jambo ambalo kila mtu anapaswa kulikumbuka na kufahamu sikuzote ni kwamba "MAGONJWA MENGI NI ROHO, CHANZO CHAKE NI ROHONI, NI KITU CHA ROHONI KUTOKA KWENYE ULIMWENGU WA ROHO"
Ndio maana utasikia watu wengine wanasema "ninaumwa kweli na nimekwenda hospitalini kupimwa hawajaona ugonjwa".
YESU ALIKEMEA homa ikamwacha, jambo hilo linatosha kuwajulisha wanadamu kuwa YESU ANAWEZA KUPONYA NA KUONDOA MAGONJWA.
Angalizo
1. Usife kizembe, kama hospitali wamepima hawajaona magonjwa KIMBILIA KWA YESU.
2. Ikitokea umeumwa jizoeze kukemea ugonjwa, nakuambia jambo ninalolifahamu sana nimewahi kupona kwa kukemea tu.
3. Sijasema ukiumwa usiende hospitali ila nimekutazamisha kwamba magonjwa mengi ni roho, ni kitu cha rohoni kutoka kwenye ulimwengu wa roho, shituka.
4. Kama haujaokoka, hakikisha unaokoka sio kwa ajili ya kwenda mbinguni tu bali ni kwa ajili ya usalama wako (kuokoka ni kinga dhidi ya mambo mengi kutoka kwa shetani).
0 Maoni