Ila Biblia inatuambia Mfalme Farao alimuweka Yusufu kwenye nafasi ile kwa kuwa aliona jambo la tofauti ndani ya Yusufu (Mwanzo 41:38), Mfalme Farao hakutaka kujua kiwango cha elimu ya Yusufu, ujuzi alionao nakadhalika ila alimpa nafasi ile kwa sababu Yusufu ana Mungu.
IKO HIVI: Haijalishi nafasi za kazi zina watu au zimejaa, yamkini kazi hazipo, yamkini ajira hazitangazwi, YUPO MUNGU MBINGUNI AWEZAYE KUWATENGENEZEA MAZINGIRA RAFIKI WATU WAKE ILI WAPATE KAZI.
●Ni Mungu aliyemtengenezea Daudi mazingira rafiki ya kupata kazi kwa Mfalme Sauli.
●Ni Mungu aliyemtengenezea Yusufu mazingira rafiki ya kupata kazi kwenye utawala wa Mfalme Farao wa Misri.
0 Maoni