HATA SHETANI HUWA ANAKWENDA KANISANI


Ukristo halisi sio kwenda kanisani kila jumapili tu au kwenda kwenye kusanyiko la kiibada BALI NI KUFANANA NA KRISTO (Mathayo 11:29).

Ukristo halisi sio kubatizwa kwa  maji mengi tu BALI NI MAISHA YANAYOMWAKILISHA KRISTO KWA JAMII (Mathayo 5:14-16).

Ukristo halisi sio kujua mistari mingi ya Biblia au kukariri maandiko tu, hata shetani anayajua maandiko (Mathayo 4:6)  UKRISTO HALISI NI KUKAA KATIKA NENO LA KRISTO NA KULIISHI.

Ukristo halisi sio kuitwa jina la kiebrania au kiyunani BALI NI KUWA NA JINA JEMA (SIFA NJEMA) KWENYE JAMII (2 Wakorintho 6:4)(Mhubiri 7:1).

NB: Hata shetani huwa anakwenda kanisani, amua kuwa mkristo halisi.

Chapisha Maoni

0 Maoni