(Luka 19:10) Yesu alisema alikuja kutafuta na kuokoa kilichopotea, mbinu mojawapo ambayo Bwana Yesu aliitumia kuwatafuta waliopotea ni kuwatembelea (visitation).
(Mwanzo 3:8-13) Mungu aliwatembelea Adamu na mkewe pale Bustani ya Edeni, alikuwa anawatafuta kwa kuwa walipotenda dhambi walipotea kwa jinsi ya rohoni ndio maana aliuliza "uko wapi?
Lengo la Mungu kuwatembelea ni kutaka kuwarejesha kwake lakini hawakukubaliana naye (hawakukiri na kutubia dhambi yao).
Kutembelea walipotea ni mbinu mojawapo ya kibiblia ya kuwatafuta watu waliopotea.
-Yesu alimtembelea Zakayo nyumbani kwake (Luka 19:5-10)
-Yesu aliwatembelea wagerasi (Luka 8:22-37)
HITIMISHO
Jukumu letu kama wakristo ni kuwatafuta walipotea na kuwarejesha kwa Mungu, mbinu mojawapo ya kuwatafuta walipotea ni kuwatembelea.
Kuwatembelea kwenye miji yao, kazini kwao, mahali wanapopatikana nakadhalika.
0 Maoni