Kuna wakati unaweza kukosewa lakini ukikaa ukatafakari unaweza kugundua kuwa wewe ndiye uliyekosea, makosa yako ndio yalisababisha ukakosewa (wengine wakakosea).
Hivyo basi usiwe mwepesi wa kulalamika, kuwanyooshea wengine vidole na kuhukumu waliokukosea.
NB: Ukikosewa, pata muda wa kutafakari kabla ya kufanya maamuzi ili ubaini kama makosa yako ndio yamesababisha wengine kukosea au la, HEKIMA NI PAMOJA KUONA AU KUTAMBUA MAKOSA YAKO SIO KUONA MAKOSA YA WENGINE TU.
0 Maoni