Ujumbe mmojawapo uliobebwa kwenye mfano huo ni KUMZALIA MUNGU MATUNDA.
Yesu alimaanisha chochote anachokupa Mungu (mali, fedha, kazi nakadhalika) anataka kimzalie Mungu matunda haijalishi ni kidogo au kikubwa (talanta nyingi au chache).
Yule aliyeshindwa kuzalisha talanta aliyopewa aliambiwa ni mtumwa mbaya na mlegevu (Mathayo 25:26)
Mtumwa mbaya na mlegevu aliambiwa kuliko kukaa na talanta asiyoweza kuizalisha NI HERI ANGEWAPA WENGINE WANAOWEZA KUIZALISHA (Mathayo 25:26-27).
Fundisho tunalopata hapo ni kwamba KULIKO KUKAA NA KITU KISICHOMZALIA MUNGU MATUNDA NI HERI KUWAPA WENGINE WANAOWEZA KUMZALIA MUNGU MATUNDA NA KITU HICHO (Mathayo 25:26-27).
Usipomzalia Mungu matunda jiandae kunyang'anywa ulichopewa na Mungu ili wapewe wengine wanaozaa matunda (Mathayo 25:28)
0 Maoni