JINSI WATU WANAVYOMSABABISHIA MUNGU HASARA NA NAMNA YA KUMSABABISHIA MUNGU FAIDA


 Yesu alipotoa mfano wa talanta (Mathayo 25:14-28) alikuwa anafundisha mambo mengi kuhusu ufalme wa Mungu.

Ujumbe mmojawapo uliobebwa kwenye mfano huo ni MUNGU HATAKI KUPATA HASARA.

Chochote ambacho Mungu anakupa anataka kimzalie matunda ili apate faida haijalishi ni kidogo au kikubwa, haijalishi ni vingi au vichache (Mathayo 25:26-27)

Kutokuzaa matunda wakati umeshapewa talanta na Mungu ni kumsababishia Mungu hasara, Mungu hafurahii watu wanaomsababishia hasara (Mathayo 25:26-27).

NB:

1. Chochote anachokupa Mungu hakikisha Mungu anapata faida sio hasara.

2. Kusababisha jina la Bwana litukuzwe au kusababisha Mungu ajipatie utukufu ni kumpa Mungu faida.

3. Kusababisha wengine wamuamini Yesu ni kumpa Mungu faida.

4. Kusababisha Mungu ajulikane katika jamii ni kumpa Mungu faida (Zaburi 76:1)

Chapisha Maoni

0 Maoni