UPANDE WA PILI WA UFUASI

 

Ufuasi una pande mbili, upande wa kwanza ni upande wa mema na upande wa pili ni upande wa mambo yasiyofurahisha.

Yaliyompata unayemfuata yatakupata wewe pia haijalishi ni mema au mabaya.

UPANDE WA PILI WA UFUASI UKO HIVI

1 Wathesalonike 2:14

Wathesalonike waliamua kuwa wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyokuwa katika uyahudi.

Mateso yaliyowapata kule kwenye makanisa ya uyahudi yaliwapata pia wathesalonike.

Marko 10:38

Yesu aliwaambia wafuasi wake kuwa kikombe atakachonywea nao watakinywea.

Alimaanisha wafuasi wake watapatwa na mateso kutokana na kuwa wafuasi wake.

Kama Yesu alikataliwa na baadhi ya watu basi na wao wangejikuta wanakataliwa na baadhi ya watu.

Kama Yesu aliinukiwa basi na wao watajikuta wanainukiwa na watu.

Kama Yesu alipingwa basi na wao watapingwa, hawatakubalika kwa watu wote.

HITIMISHO

Ufuasi utakufanya upate mema na utakufanya ukumbane na mambo yasiyofurahisha.

Hiyo ni kanuni ya ufuasi isiyoweza kuepukika.

Kama umeamua kuwa mfuasi wa Yesu au mfuasi wa mtumishi fulani wa Mungu basi yaliyompata unayemfuata yatakupata na wewe haijalishi ni mema au mabaya.

Upande wa mabaya watu huwa hawautazami sana ila upo, ndio maana kuna wakati Yesu alisema ukitaka kuwa mfuasi wake lazima ujikane nafsi yako na uubebe msalaba wako kila siku halafu umfuate (Luka 9:23).

NB: Japo mabaya yapo lakini Mungu anasema USIOGOPE.


Chapisha Maoni

0 Maoni