Hata Bwana Yesu alizungumzia maneno hayo mawili "ndiyo na siyo"
Mathayo 5:37.
Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.
---------------
But let your 'Yes' be 'Yes,' and your 'No,' 'No.' For whatever is more than these is from the evil one.
Umuhimu mmojawapo wa maneno hayo ni kwamba hayo maneno "ndiyo na hapana" yanaweza kukupa ushindi dhidi ya aina fulani ya majaribu.
Kupitia chapisho hili nitafundisha kuhusu neno hapana na jinsi lilivyowasaidia baadhi ya watu.
BAADHI YA MIFANO YA NENO "HAPANA" ILIVYOWASAIDIA BAADHI YA WATU KUSHINDA MAJARIBU
MFANO WA 1: (Mwanzo 39:7-12)
Yusufu alitamaniwa na mke wa bwana wake (mke wa mwajiri wake) lakini Yusufu alisema HAPANA.
Kilichomuokoa Yusufu sio maombi, sio sadaka, sio kufunga, sio unabii, sio nasaha bali ni HAPANA (ALISEMA HAPANA).
MFANO WA 2: (Danieli 3:1-26)
Hao vijana watatu walishinda jaribu la kuabudu miungu kwa kusema HAPANA (HATUTAABUDU MIUNGU).
Hawakufunga na kuomba, hawakutoa sadaka ili Mungu awatetee ila WALISEMA HAPANA.
HITIMISHO
Yakobo 5:12.
Lakini zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, wala kwa mbingu wala kwa nchi; wala kwa kiapo kinginecho chote; bali ndiyo yenu na iwe ndiyo, na siyo yenu iwe siyo, msije mkaangukia hukumu.
---------------
But above all, my brethren, do not swear, either by heaven or by earth or with any other oath. But let your "Yes," be "Yes," and your "No," "No," lest you fall into judgment.
0 Maoni