SABABU YA 1: KWA KUWA UNA MWILI
(Mathayo 26:41)
Yesu aliwaambia wanafunzi wake kwa nini walipaswa kuomba ni kwa sababu wana miili.
Unaweza kujiuliza kwani mwili una shida gani?
a). Mwili unashindana na Roho, mwili hauyataki mambo ya Mungu (Wagalatia 5:17), roho iko tayari ila mwili hautaki (Mathayo 26:41)
b). Mwili unaweza kusababisha usifanye unayotaka (Wagalatia 5:17) yaani mambo ya kiungu.
c). Mwili unaweza kusababisha ukakosa kuingia mbinguni (Wagalatia 5:19-21)
SABABU YA 2: ILI USIBAKI NJIA PANDA KIMAAMUZI
(Matendo ya mitume 1:24-26)
Wanafunzi wa Yesu walijikuta wako njia panda kimaamuzi wakashindwa kuamua kwa haraka nani achukue nafasi ya Yuda, walitaka kumpata mtu wa kukaa kwenye nafasi ya Mtume Yuda Iskariote.
Walichukua hatua ya kumwomba Mungu kisha wakawapigia kura watu wawili na mmoja wao akachaguliwa kutwaa nafasi ya Yuda.
IKO HIVI: Kuna wakati watu hujikuta wako njia panda hawajui waamue nini, ni vema ufahamu kuwa maombi yanaweza kukusaidia kutoka njia panda.
SABABU YA 3: KWA SABABU WEWE NDIO UNAJUA MAUMIVU UNAYOYAPATA KUTOKANA NA YANAYOKUSUMBUA
(Mathayo 26:37-39)
Yesu aliwaambia roho yangu ina huzuni kiasi cha kufa kisha akawaambia wanafunzi wake waombe lakini hawakuomba.
IKO HIVI: Ukitegemea kuombewa na wengine unaweza kujikuta hausaidiki kwa chochote, wewe ndio unajua maumivu unayopata kutegemeana na yanayokukumba lakini mtu mwingine hajui, anayeweza kuyabeba hayo mambo kwa mzigo mbele za Mungu ni wewe.
Yesu aliomba mwenyewe hakutegemea maombi ya wakina Petro, angeyategemea maombi ya wakina Petro wasioomba unahisi nini kingetokea?
(1 Samweli 1:9-20)
Kule hekaluni alikuwepo kuhani Eli lakini yule mwanamke aitwaye Hana hakuyategema maombi ya kuhani Eli, aliomba yeye mwenyewe maana yeye ndiye alikuwa anajua maumivu anayoyapata kutokana na kukosa mtoto.
HITIMISHO
Katika sehemu ya kwanza nilifundisha sababu tano kwa nini unapaswa kuwa mwombaji, unaweza kufuatilia somo hilo kupitia kiunganishi hiki
https://maarifatime.blogspot.com/2025/02/sababu-5-kwa-nini-uwe-mwombaji.html
0 Maoni