KUTOKUSAMEHE NI SAWA na kubanwa na mkojo au kinyesi lakini hautaki kuingia chooni kukitupa hicho kinyesi au kuachia huo mkojo.
Ukijizuia kukojoa au kutupa kinyesi tarajia kuaibika kwa kuwa utajinyea au kujikojolea.
KUTOKUSAMEHE NI SAWA na kutunza uchafu moyoni mwako.
KUTOKUSAMEHE NI SAWA NA kusafisha nyumba halafu ukakusanya uchafu na kuhifadhi kwenye jokofu.
IKO HIVI, unayeumia ni wewe ikiwa utashindwa kusamehe, usiendelee kukaa na uchafu moyoni, TUPA HUO UCHAFU.
AMUA KUSAMEHE SASA.
0 Maoni