KIBALI CHA MUNGU


UTANGULIZI

Hapa duniani kuna mambo ambayo huwezi kuyafanya kama hauna kibali cha serikali au mamlaka mbalimbali.

Kwa mfano ukitaka kujenga utatakiwa kuwa na kibali cha ujenzi.

Ukitaka kufanya biashara fulani utatakiwa kuwa na vibali.

Huwezi kumtoa mtu hospitalini bila kupata kibali kinachomruhusu kutoka hospitali.

VIVYO HIVYO

Kuna mambo hayatatokea kwenye maisha yako, kuna vitu hautavipata bila kibali cha Mungu.

(Mwanzo 39:21)

Mungu alimpa Yusufu kibali, kile kibali kilimsaidia mambo mengi ikiwemo kupata nafasi ya kuwa mkuu wa wafungwa.

(Kutoka 11:3)

Mungu aliwapa kibali waisraeli, kile kibali kiliwasaidia mambo mengi ikiwemo kutoka Misri.

(1 Samweli 2:26)

Samweli alipata kibali cha Mungu, kibali kilimsaidia mambo mengi ikiwemo kusikilizwa na watu.

AINA ZA VIBALI VYA MUNGU

Nilitangulia kusema hapa duniani kuna aina mbalimbali za vibali kama vile vibali vya ujenzi, biashara, usafiri nakadhalika.

Vivyo hivyo Mungu ana vibali vya aina nyingi, baadhi ya vibali vya Mungu ni;-

1. KIBALI CHA KUSIKILIZWA 

(Danieli 1:9-15)

Mungu alimpa kibali Danieli, kibali kilisababisha akasikilizwa hoja yake (jambo lile lisingewezekana bila kibali cha Mungu).

(Nehemia 2:5-9)

Mungu alimpa kibali Nehemia, mambo aliyomwambia Mfalme aliyasikiliza na akayakubali, kibali cha Mungu kilimsaidia mambo mengi ikiwemo kupata vitu anavyotaka ili kutimiza jukumu lililokuwa mbele yake.

2. KIBALI CHA KUKUBALIKA

(Esta 2:15-17)

Biblia haisemi Esta alikuwa mrembo kuliko mabinti wengine ila kibali cha Mungu kilisababisha akakubalika.

3. KIBALI CHA KUFANYA KAZI FULANI

-Musa alipata kibali cha kuwatoa wana wa israeli kutoka Misri.

-Gideoni alipata kibali cha kuwaokoa wana wa Israeli dhidi ya mikono ya wamidiani.

FAIDA KADHAA ZA KIBALI CHA MUNGU

1. Kibali kinaweza kusababisha mtu akapata nafasi (fursa fulani)

(Mwanzo 39:21) Yusufu alipopata kibali cha Mungu kilimsaidia kupata nafasi (fursa) kule gerezani.

2. Kibali kinaweza kusababisha mtu akapata vitu anavyotaka.

(Nehemia 2:5-9) Kibali cha Mungu kilimsaidia Nehemia kupata vitu vilivyomsaidia kutimiza jukumu alilopaswa kulitimiza.

NAMNA YA KUPATA KIBALI CHA MUNGU

1. Muombe Mungu akupe kibali (Mathayo 7:7)

2. Tenda vema sawasawa na neno la Mungu.

(Mwanzo 4:7) 

3. Tii neno la Mungu (Mithali 3:1-4)

HITIMISHO

Yapo mambo mengi ya kujifunza kuhusu kibali cha Mungu, nimefundisha hayo ili kukuwekea msingi wa kujifunza zaidi.

Chapisha Maoni

0 Maoni