BAADHI YA MAMBO YANAYOSABABISHA MAOMBI YAWE NA NGUVU



1. KUOMBA KWA MZIGO.
-Kuomba kwa mzigo ni kuomba kwa kumaanisha kabisa kutokana na kutoridhishwa na jambo lililotokea au linaloendelea.

(Matendo ya mitume 12:1-5)
Mtume Yakobo alikamatwa akauawa hatuoni kanisa linamuomba Mungu lakini alipokamatwa Mtume Petro ndipo kanisa likaanza kuomba kwa mzigo hatimaye malaika alitumwa kumtoa gerezani.

(1 Samweli 1:1-20)
Kutokana na kutokuwa na mtoto, Hana aliomba kwa mzigo sana hakuridhika na kuendelea kukosa mtoto ndio maana aliomba kwa mzigo sana hatimaye alipata mtoto.

2. KUOMBA KWA IMANI.
(Yakobo 5:15)
Kuomba kwa imani ni kuomba huku una uhakika kuwa unayoyaomba Mungu anayasikia na atayajibu (Marko 11:24)

Kuomba kwa imani ni kuomba sawasawa na neno la Mungu, huwezi kutenganisha imani na neno la Mungu kwa kuwa imani chanzo chake ni kusikia neno la Mungu (Warumi 10:17)

3. KUOMBA HUKU UKIWA NA HOJA ZENYE NGUVU.
(Isaya 41:21)
Mungu anataka hoja zenye nguvu katika maombi yako.

Kwa mfano Mungu alitaka kuwaua waisraeli lakini hoja ya Musa ilisababisha Mungu akaghairi kuwaua waisraeli (Kutoka 32:9-14)

Hoja ya Musa ilijengwa kwenye agano la Mungu kwa Ibrahimu, Isaka na Yakobo, laiti kama Mungu angewaua waisraeli angekuwa amevunja agano lake ndio maana aliacha kuwaua.

Hoja ya Mfalme Hezekia ilisababisha Mungu akamuongezea miaka kumi na tano ya kuishi (Isaya 38:1-6)

Hoja ya Mfalme Hezekia ilijengwa kwenye utumishi wake, alimkumbusha Mungu namna alivyomtumikia, Mungu akamuongezea miaka na akamponya.

4. KUOMBA SAWASAWA NA MAPENZI YA MUNGU.
(1 Yohana 5:14-15)

Ili uweze kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu lazima uwe na ufahamu unaotokana na neno la Mungu au uwe na neno la Mungu ndani yako pia lazima ukubali kuongozwa na Roho Mtakatifu katika kuomba.

Chapisha Maoni

0 Maoni