FURAHA YA KURUDI NYUMBANI


 Tulipokuwa shule ya msingi, wanafunzi walikuwa wanafurahi zinapopigwa kengele za aina mbili.

1. Kengele ya wakati wa kupumzika.

2. Kengele ya wakati wa kuondoka shuleni.

Wakati tunaondoka shuleni tulikuwa na furaha kubwa kwa kuwa tunarudi nyumbani ambapo tutakula chakula na tutakuwa huru kutembea huku na kule.

Kuwa mbali na mazingira ya nyumbani kulisababisha tusipate vitu fulani na uhuru wa kutosha lakini tuliporudi nyumbani tulikuwa huru kwenda kutembeatembea huku na kule na kupata chakula.

Kurudi nyumbani kulisababisha furaha kwetu na kwa wazazi kwa kuwa tuliporudi nyumbani wazazi walitutuma kule walikotaka kututuma.

IKO HIVI

Unajua ukiwa nje ya Yesu Kristo uko mbali na pia uko nje ya nyumbani kwenu?

Unajua kuna vitu unakosa na kuna uhuru unakosa kwa kuwa uko mbali na uko nje ya nyumbani kwenu?

(Luka 15:11-24)

Kijana ambaye habari zake zimeandikwa hapo alijikuta yuko kwenye mateso kwa kuwa alikuwa mbali na nyumbani.

Alipoamua kurudi nyumbani alipata furaha pia alisababisha furaha kwa watu wengine ikiwemo baba yake.

Kurudi nyumbani kulibadilisha kabisa maisha yake.

NI WAKATI WA KURUDI NYUMBANI

Ukirudi nyumbani (ukiingia ndani ya Yesu Kristo) utapata furaha, uhuru na mambo mengine unayopaswa kuyapata kama mtoto wa nyumbani mwake Mungu.

"hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Yesu Kristo amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya" 2 Wakorintho 5:17

Chapisha Maoni

0 Maoni