JE! NI SAHIHI KUVAA NGUO ZA MTUMBA?


 
UTANGULIZI

Nguo za mtumba ni nguo ambazo zimekwisha kuvaliwa na mtu mwingine halafu mtu mwingine akaamua kuzivaa.

Watu huzipata nguo za mtumba kwa njia kama tatu
●Kununua.
●Kupewa na ndugu, jamaa au rafiki.
●Kurithi, kwa tamaduni nyingi za waafrika akifa baba, mama, mlezi au mtu wa karibu, watu hupewa nguo zake kama sehemu mojawapo ya urithi.

SUALA LA UVAAJI WA MITUMBA KIBIBLIA

(Kutoka 3:22)
Ukisoma andiko hilo utaona Mungu akiwaambia wanawake wa kiebrania (waisraeli) wawaombe wamisri vito vya thamani pamoja na MAVAZI.

Kwa mantiki hiyo ni sawa na kusema kwamba MUNGU ALIWARUHUSU WATOTO WA KIEBRANIA WAVAE MTUMBA.

UNACHOPASWA KUFAHAMU KUHUSU MAVAZI KIBIBLIA

Mavazi ya mtu yanaweza kubeba roho fulani au nguvu za kiroho za shetani au za Mungu.

Kwa mfano
●(2 Wafalme 2:13-14)
Nabii Elisha alipiga maji ya mto Yordani kwa vazi la Nabii Elia maji yakagawanyika kisha akavuka.

Mavazi ya Nabii Elia yalikuwa na nguvu za Mungu zilizogawanya yale maji ya mto Yordani.

● (Luka 8:44)
Mwanamke aliyekuwa anatokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili alipogusa upindo wa vazi la Yesu alipona ule ugonjwa.

Mavazi ya Yesu yalikuwa na nguvu zilizosababisha uponyaji.

JE! NI SAHIHI KUVAA NGUO ZA MTUMBA?

1. Aliyetoa maelekezo ya kuwavalisha nguo za mtumba watoto wa kiebrania ni Mungu (Kutoka 3:22)

Hivyo basi ni sahihi kuvaa nguo za mtumba ikiwa Mungu hajakuzuia na ikiwa amani ya Kristo inaamua hivyo moyoni mwako.

2. Ikiwa utanunua nguo, utapewa nguo au utarithi nguo HAKIKISHA UNAZITAKASA KWA DAMU YA YESU KRISTO.

Angalizo: hata nguo ambazo sio za mtumba ni muhimu kuzitakasa ili zikufae.

HITIMISHO
Suala la uvaaji wa mavazi ni pana sana kibiblia, nimefundisha mambo machache ya kukusaidia hususani katika uvaaji wa nguo za mtumba ili ufahamu kweli itakayokuweka huru.

Chapisha Maoni

0 Maoni