(LUKA 18:1-6)
Yesu alitoa mfano wenye umuhimu sana katika maisha ya maombi.
Ukitafakari mfano huo utafahamu mambo mengi sana kuhusu maombi, jambo mojawapo ni hili
"hautapata haki zako kirahisi"
Kuna mambo ni haki yako kabisa unapaswa utendewe lakini hayatatokea kirahisi.
LAZIMA uombe bila kukoma mpaka utakapopata haki zako, wekeza kwenye maombi ili uzipate haki zako (LUKA 18:7-8).
Yule mjane asingeng'ang'ana asingepata haki yake ila kilichomsaidia kupata haki yake ni kung'ang'ana kwenye kudai haki yake.
0 Maoni