AMINI TU


 Daudi ambaye tunamtambua kama Mfalme wa pili wa wana wa Israeli wakati akiwa katika harakati za kukabiliana na Goliathi

●Hakuwa na elimu rasmi.

●Hakuwa na cheti cha taaluma yoyote.

●Alikuwa mdogo kiumri.

●Hakuwa na mafunzo rasmi ya kijeshi.

●Hakuwa anajulikana.

●Hakuwa na mvuto.

●Hakuwa na pesa.

●Hakuwa na mali.

ILA alikuwa na imani.

Imani ilimsaidia kupata ujasiri wa kumkabili na kumuangamiza Goliathi.

Imani ilisababisha akawa maarufu.

Imani ilisababisha akapata mke.

Imani ilimtengenezea mvuto.

Imani ilisababisha akaketi pamoja na wakuu.

IMANI inaweza kukupeleka mahali ambapo si rahisi kufika kwa namna ya kawaida, imani inaweza kusababisha jambo lolote jema kutokea kwenye maisha yako.

AMINI TU.

Chapisha Maoni

0 Maoni